
Nchi zenye viwango vya chini vya utoaji wa huduma kwa kawaida zinafanana katika jambo moja: upungufu au ukosefu wa maandalizi kuhusu vikwazo au uthawabishaji. Kwa hiyo hata kama demokrasia inatazamwa kama dhana inayohusisha taratibu za uwajibikaji, hali halisi inatatanisha zaidi. Kuna vipengele vingi vinavyoathiri utoaji wa huduma na namna taratibu za uwajibikaji zinavyofanya kazi. Mara nyingi njia hizo huwa hazipo kabisa, hazifai au zinazobagua kwa misingi ya utambulisho wa mtu, mwelekeo wa kijinsia, umri, kipato, ulemavu au nguvu ya mtu kijamii.
Mwongozo huu una mbinu za tathmini zinazotumika kubainisha maboresho katika njia za uwajibikaji wa kidemokrasia. Mfumo huu ni nyongeza mpya kwenye mkusanyiko wa mifumo ya tathmini inayoongozwa na wananchi wa International IDEA: Hali ya Demokrasia na Hali ya Tathmini ya Demokrasia katika Jamii Husika. Watumiaji wa mwongozo huu wataweza kubainisha iwapo wahusika wanaweza kuwajibika katika kila hatua ya mchakato wa sera juu ya utoaji wa huduma za umma, na pia jinsi ya kuboresha njia hizo za uwajibikaji.

Contents
Dibaji
Akronimi na Vifupisho
Utangulizi
1. Dhana za Tathmini
2. Mfumo wa Tathmini
3. Mchakato, Hatua Muhimu na Mtiririko wa Kazi ya Tathmini
Maelezo